top of page

Sisi ni nani

20200228_131816.jpg

The WASH SDG

Mradi wa WASH SDG unalenga katika kuboresha huduma safi kwenye mnyororo wa usafi wa mazingira mjini. Mradi huu umefadhiliwa na serikali ya Uholanzi (DGIS), huku ukiwa na lengo la kuunga juhudi za upatikanaji salama wa huduma za usafi wa mazingira na kuboresha matendo bora ya usafi kwenye jiji la Arusha na Manispaa ya Shinyanga (2017-2022).

 

Ili kutimiza haya, mradi huu unaweka mkazo kwenye maeneo matatu tofauti; kuboresha mabadiliko ya tabia yatakayoleta uhitaji wa  kuboresha vifaa tumika katika eneo la usafi wa mazingira na kuvitumia kwa usahihi; kuboresha utowaji huduma utakaopelekea upatikanaji na uwezo wa kupata bidhaa zinazotumiwa, na huduma ambazo zitachangia uendelevu na usawa kwenye eneo la usafi wa mazingira; Kuimarisha utawala utakaopelekea serikali kuwezesha ufanisi kwenye utowaji wa huduma ambao unachangia uendelevu na usawa wa kupata huduma za usafi wa mazingira.

Arusha City Council

Inalenga kutoa huduma endelevu kwa kushirikia na wadau ili kuongeza uwezo wa jamii yenye tamaduni nyingi kuendeleza na kukuza uchumi endelevu, ustawi wa jamii na mazingira kupitia utawala bora.

Shinyanga Municipal Council

Maono na mikakati ya halmashauri hii, ni kuhamasisha amani, usalama na utawala bora, ili kutoa huduma bora kwa wananchi na kutengeneza mazingira mazuri ya kuimarisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wananchi.

AUWSA

Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Jijini Arusha hupanga, hukuza na kuendeleza mfumo wa maji taka katika kuhakikisha ukusanyaji na utupaji salama wa maji taka, Pia kuweka tozo halisi za maji safi na maji taka, na hivyo kukusanya mapato kutokana na matumizi ya maji safi na ukusanyaji wa maji taka kutoka kwa wateja.

SHUWASA

Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Shinyanga inatoa huduma bora na ya ufanisi ya usambazaji wa maji safi na usafi wa mazingira kwa wateja wake ndani ya Manispaa ya Shinyanga, na kujivunia wafanyakazi wenye motisha, ujuzi, uwezo, kujitoa na wenye bidii wakati wa kutumia teknolojia mahususi zilizo rafiki kwa mazingira.

kouPnseq3bRAWR.jpeg

Kuhusu SNV

SNV ni shirika la kimataifa la kimaendelea linalolenga katika kuboresha maisha ya watu wanaoishi kwenye umaskini kwa kuwasaidia kuongeza vipato vyao na kupata huduma muhimu. Tunalenga kwenye sekta kuu tatu (Maji, kilimimo na nishati) na tupo kwenye Zaidi ya nchi 25 zilizopo Asia, Africa na Latin Amerika. Timu ya wafanyakazi zaidi ya 1300 ndio uti wa mgongo wa SNV.

bottom of page