top of page

Unyonyaji salama na kwa wakati wa maji taka

Weka mkakati kabla

Weka mkakati wa kunyonya choo chako kabla hakijafurika kwenda kwenye mazingira na kuhatarisha jamii yako. Tunza taarifa kwenye Kalenda ili kujua lini ulinyonya na/au fanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye shimo la choo kuhakikisha halifuriki.

Weka akiba

Weka kidogo akiba pembeni na wekeza hela za kaya kwa ajili ya kuboresha choo. Kwa kunyonya salama na kwa wakati wa choo chako na kutotupa taka ngumu kwenye shimo la choo, utaweza kuokoa pesa na kujilinda dhidi ya magonjwa, kuepuka kupigwa faini na kulipa fedha Zaidi kwa ajili ya kutoa taka ngumu kwenye choo chako.

Wapigie watoa huduma walioidhinishwa

Tumia watoa huduma walioidhinishwa kwa ajili ya kunyonya choo cha kaya yako. Hakikisha wanavaa vifaa kinga (Glovu, Mabuti, nguo maalumu, Barakoa,kofia na miwani) na kuweka mazingira safi na kuepuka kupigwa faini.

Scene-4-Facebook_edited.jpg

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Kwanini ni muhimu kuwatumia watoa huduma walioidhinishwa?

Ukiachana na watoa huduma wasioidhiniwa, watoa huduma walioidhinishwa wamepewa leseni na halmashauri za mji ambao wanaweza kunyonya choo chako kitaalamu kwa maana kwamba, watatumia vifaa kinga (Glovu, Mabuti, nguo maalumu, barakoa, kofia na miwani) na kuilinda familia na jamaii yako kutoka kwenye magonjwa ya mlipuko yanayotokana na kazi za kunyonya maji taka.

Je, ni mara ngapi natakiwa kunyonya shimo la choo au tenki?

Kwa kawaida, mashimo na tenki za choo hutumia miaka mitatu hadi mitano kujaa. Hata hivyo, inategemea na idade ya watumiaji. Ili kupata taarifa sahihi za hali yako, unaweza kupiga simu kutokana na eneo ulilopo (Arusha +255 and Shinyanga 0800 711 102 na hivyo watakadiria ni mara ngapi utahitaji kunyonya choo chako au tenki lako. Baada ya makadirio kufanyika, na kujua ni muda gani inachukua, tunakushauri uwe unafanya ukaguzi  w achoo/tenki lako ili kuhakikisha halifuriki.

Unajuaje kwamba huu ni wakati sahihi wa kunyonya choo/ tenki lako?

Choo/Tenki lako linatakiwa kunyonywa ikiwa imebakia sentimita 10 kujaa. Kujua hili unaweza kupiga simu kutokana na eneo ulilopo (Arusha 0800 110 069 and Shinyanga 0800 711 102 na watakadiria urefu na mara ngapi unatakiwa unyonye choo au tenki lako. Baada ya kufanyika kwa makadirio haya, na kujua ni wakati kwa kawaida inachuku, tunakushauri ufanya ukaguzi kwa kuangalia mara kwa mara mwezi mmoja kabla ya kunyonya choo chako ili kisifurike

Ni gharama kiasi gani, kutumia watoa huduma walioidhinishwa?

Watoa huduma wa umma wanagharimu kuanzia 65.000 hadi 95.000 TZS kutegemea na umbali, na watoa huduma binafsi wanagharimu kuanzia 60.000 hadi 120.000 TZS kutegmea na umbali (kutoka kwenye nyumba hadi sehemu ya kumwaga)

Ni muda gani uchukua toka ninapopiga simu kuomba huduma ya kunyonya choo kutoka kwa watoa huduma walioidhishwa?

Mara baada ya kuwapigia simu watoa huduma walioidhinishwa, huwa wanachukua kuanzia kufika kwenye nyumba yako. Halafu, mara baada ya kufika nyumbani kwako, huchukua kuanzia 30-45 min kunyonya choo/tenki lako.

Nitakuwa nina uhakika gani kwamba wamenyonya kitaalamu?

Kuna orodha ya ukaguzi unaweza kuomba kutoka kwa mtoa huduma wanapokuja kwa huduma ya unyonyaji. Orodha ya ukaguzi inajumuisha utumiaji sahihi wa vifaa kinga, kusafisha mazingira baada ya kunyonya na kutumia vifaa vya kitaalamu.

Ni nani natakiwa kumpatia tarifa, ikiwa nimemuona mtu ananyonya kinyume na sheria?

Unaweza kupiga simu hii kutoka kwenye eneo lako (Arusha 0800 110 069 and Shinyanga 0800 711 102 na watahakikisha wanachukua hatua dhidi ya mtu na/au mtoa huduma anayenyonya kinyume na sharia.

bottom of page