Utunzaji salama wa taka ngumu
Weka pipa/ kifaa cha kutunza taka
Weka pipa au kifaa cha kutunzia taka ndani ya chumba cha choo kwa ajili kutunzia taka ikiwemo taulo za kike. Kamwe usitupe taka ngumu ndani ya shimo la choo, kwani kitendo hiki kinaweza kusababisha choo kuziba na kufurika. Tupa takataka kwenye pipa.
Weka pipa sehemu maalumu
Tenga sehemu maalumu kwenye eneo la kaya yako na uweke pipa/ chombo cha kutunzia taka chenye mfuniko kwa ajili ya kutunza taka hadi pale wakusanyaji taka watakapokuja kwa ajili ya kukusanya.
Kukusanya
Wape watoza huduma kipato cha taka kwa wakati uliopangwa au ikiwa wameidhinishwa (shule na vituo vya afya) kuchoma taka ngumu kwa vyombo vya moto.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Kwanini ni muhimu kutupa taka kwenye vyombo vya kutunzia na sio kwenye shimo/tenki la choo?
Taka ngumu kama taulo za kike, nepi, nguo, magazeti, plastiki na nyingine zinazotupwa kwenye mashimo ya choo, zinasababisha vyoo/tenki kuziba na kuongeza mzunguko wa kunyonya choo chako, kwani kinajaa haraka na kuongoza gharama za unyonyaji kwani gharama ya ziada inatoozwa kwa kuondoa taka ngumu kabla ya kuanza kunyonya- kitu kinachoongeza gharama za unyonyaji kwako. Pia, inaongeza nafasi kubwa kwa kusambaa kwa magonjwa ambayo yanahatarisha afya ya familia na jamii yako.
Natakiwa kufanya nini na taka nilizotupa kwenye pipa la kutunzia taka?
Kaya zinatakiwa kuchukua taka zilizotupwa kwenye chombo maalumu cha kutunzia taka/pipa na kuchanganya na takataka nyingine zilizotunzwa kwenye eneo la kaya, taka zote hizi zitatunzwa/kutupwa sawa.
Uhifadhi na utupaji salama wa taka ngumu ni nini?
Utunzaji na utupaji salama wa taka ngumu unamaanisha ni kitendo ccha kuweka pipa/chombo cha kutunzia taka chenye mfuniko ndani ya chumba cha choo ambapo taka zikijaa zitahamishwa kwenye chombo kingine kikubwa zaidi kilicho nje ya choo (ndani ya eneo la kaya yako, hakikisha kina mfuniko ili kuzuia wanyama wanaofukua uchafu kama Mbwa) na kuchanganywa pamoja. Pia hakutakiwa kuwa na uvujaji wa majimaji kutoka kwenye taka ambayo yanaweza kuchafua mazingira yaliyokuwa karibu.