top of page

Kunawa mikono kwa sabani

Nyakati muhimu za kunawa mikono

Kuna nyakati tano muhimu za kunawa mikono kwa sabuni, ambazo zinapendekezwa na mamlaka na taasisi mbalimbali kama, WHO. Nyakati hizi ni kunawa mikono unaposhika uchafu, baada ya kutoka chooni, kabla ya kula, kabla ya kuandaa chakula na kunawa mikono kabla na baada kuingia ama kutoka kwenye majengo kama shule au hospitali.

jhi.jpg

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Je, mara zote huwa unahitaji kuwa na sabuni pale unapotaka kunawa mikono?

Ndio, sabuni ni kitu muhimu wakati wa kunawa mikono kwa kuwa inatoa kabisa uchafu na vimelea vya magonjwa ambavyo pengine unakuwa umeshika. Kama huwezi kupata sabuni unaweza kutumia majivu.

Je, Natakiwa kufanya nini pale ninapokosa kabisa sabuni na maji?

Kama hauna maji ama sabuni karibu, unaweza kutumia kitakasa mikono 

Nawezaje kuosha kwa usalama mikono yangu?

Kwa mujibu WHO, unatakiwa kulowanisha mikono yako kwanza, halafu weka sabuni na paka eneo lote la kiganja cha mkono, halafu sugua sehemu zote za mikono, anza na kiganja cha na juu ya kiganja cha mkono wa kulia, halafu kushoto (huku ukifunga vidole vyako), sugua sehemu ya ndani ya vidole, halafu sehemu ya nyuma ya vidole, halafu sugua vidole gumba (anza na kushoto halafu kulia) endelea kusugua kila sehemu, halafu suuza kwa maji safi, halafu kausha kwa kutumia taulo/tishu malizia kwa kutumia taulo/tishu kufunga bomba.

​Kanyaga Kanyaga hand-washing station

Kituo cha kuosha mikono kwa kukanyaga na mguu ni rahisi, gharama nafuu amabayo inasaidia kuzuia kuenea kwa magonjwa na inasaidia afya ya jamii na ni sehemu ya kisasa. Hiki kituo cha kuosha mikono ni gharama nafuu, rahisi kutumia, kinazuia uchafu wa mikono, inavutia watumiaji, inapunguza matumizi ya maji na maji machafu yanaweza kuelekezwa. Pata kituo cha kanyaga kanyaga kwa ajili ya biashsara yako ama matumizi ya myumbani kuanzia 250,000sh kwa kupiga simu 0712660724.

mazingra-safi.jpg
bottom of page