top of page

Tuzilinde jamii zetu. Pamoja tunaweza.

Tabia salama za usafi wa mazingira ni zile tabia ambazo zitakuweka wewe, família yako na jamii yako salama mbali na magonjwa. Tabia salama za usafi wa mazingira zinajumuisha unyonyaji salama na kwa wakati wa maji taka, utunzaji salama wa taka ngumu, kunawa mikono kwa sabuni na utunzaji salama wa taulo za kike.

Scene-4-Facebook_edited.jpg

Unyonyaji salama na kwa wakati wa maji taka

Scene-1-Facebook_edited.jpg

Utunzaji salama wa taka ngumu

jhi.jpg

Kunawa mikono kwa sabani

Scene-2-Facebook_edited.jpg

Utunzaji salama wa taulo za kike

Nawezaje kuunga mkono tabia salama za usafi wa mazingira kwenye jamii yangu?

Ili kuunga mkono tabia njema za usafi wa mazingira kwenye jamii yako, unaweza kuanza kujifunza kwa kujifunza kuhusu tabia hizo na matendo yanaweza kuifanya familia na jamii  yako kuwa salama. Lakini pia unaweza kushiriki kwenye mikutano ya kijamii kila siku ili kuhakikisha kila mmoja anakuwa na uelewa wa namna gani anaweza kufanya tabia salama za ufasi wa mazigira. Kwa kuongezea, kuna vifaa mbalimbali vya mawasiliano tulivyotengeneza unavyoweza kuvipata kwenye “Resources” ambavyo unaweza kuvipakua na kuwatumia Rafiki zako kwa njia ya WhatsApp.

Nawezaje kutoa taarifa, ikiwa jirani yangu anafanya tabia zinazoweza kuhatarisha afya zetu?

Ikiwa umemuona mmoja wapo wa majirani au Rafiki zako anafanya tabia hatarishi kwa afya na ustawi wa familia na jamii yako, unaweza kutoa taarifa ya mtu huyo kwa kupiga namba hizi kutokana na eneo ulilopo (Arusha 0800 110 069 na Shinyanga 0800 711 102) au kwa kupiga simu kwa maafisa wa serikali (Afisa Afya, Mtendaji wa Kata au Mtaa) kutoka na mtaa uliopo. Watakuwa na furaha kuchukua malalamiko yako na kutafuta njia ya kuilinda jamii yako.

Naweza kushiriki vipi kampeni ya Mazingira Safi Maisha Bora?

Kuna njia mbalimbali za kuweza kushiriki kampeni hii ya Mazingira Safi Maisha Bora. Unaweza kuhudhuria mikutano mbalimbali iliyopo kwenye jamii yako inayochapishwa kwenye tovuti, unaweza kupakua na kusambaza vifaa vya mawasiliano, unaweza kujiunga kwenye gazeti la kila miezi ili uwe wa kwanza kupata taarifa linapotoka, unaweza kutufuata kwenye mitandao ya kijamii na unaweza kuwasiliana na sisi na ukapendekeza mawazo yako!

Ni nani anahusika kwenye kampeni ya Mazingira Safi Maisha Bora na nani anaongoza?

Kampeni hii inaendeshwa na Halmshauri ya Jiji la Arusha, Manispaa ya Shinyanga, Mamlaka za maji safi na maji taka za Arusha na Shinyanga mjini pamoja na Shirika la Maendeleo la Uholanzi.

bottom of page