top of page

Utunzaji salama wa taulo za kike

Jivunie

Jivunie hedhi yako. Kuwa kwenye kipindi cha hedhi ni kawaida, na haikupasi kuona aibu. Jivunie na utupe salama bidhaa za hedhi zilizotumika. Kwa namna unavyofanya hivi ndivyo utakavyohamasisha wanawake wengine nao wafanye.

Utupaji salama

Weka pipa/chombo cha kutunzia taka ndani ya chumba cha choo, sawa tu na kile cha kuwekea taka ngumu, kwa ajili ya kutupa kwa usalama bidhaa za hedhi kama taulo za kike na tampons.

Wezesha wanawake

Sambaza ujumbe huu ma hakikisha wanawake wengine wanajivunia hedhi zao na kuwa makini na utupaji salama wa bidhaa za hedhi.

Scene-2-Facebook_edited.jpg

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Je natakiwa kufanya nini, pale bidhaa za hedhi zinapokuwa zimetupwa kwenye pipa/chombo maalumu cha kutunzia taka?

Kwanza, weka taulo za kike zilizotumika kwenye pipa lililopo ndani au karibu na choo. Pili, kila siku hamisha taulo za kike kutoka kwenye chombo kilichondani ya choo au karibu na choo kwenda kwenye chombo/pipa kubwa zaidi lililo nje au mbali kidogo na choo chako, ili kupunguza harufu mbaya ndani ya choo. Tatu, unaweza kuzichoma kwa usalama katika tanuru (hii ni kwa maalumu kwa shule na vituo vya afya). Pia unaweza kuzikabidhi bidhaa za hedhi kwa wakusanyaji taka walioidhinishwa pamoja na taka taka nyingine zilizopo kwenye kaya yako.

Kwanini nitupe bidhaa za hedhi kwenye pipa/chombo maalumu cha kutunzia taka na si kwenye shimo la choo/tenki?

Kutupa bidhaa za hedhi kama taulo za kike, vitambaa na tampons kwenye shimo la choo kunachangia kuziba, kunyonya choo chako mara kwa mara kwa kuwa shimo/tenki la choo hujaa haraka hivyo kuongeza gharama za unyonyaji kwani itahitaji kuondoa taka ngumu ndani ya shimo la choo kabla ya kunyonya-vitu ambavyo vinaongeza gharama za kunyonya. Pia hueneza magonjwa ambayo ni hatari kwa familia na jamii yako. Kumbuka, bidhaa za hedhi hazitakiwa kuonewa aibu na hutakiwi kuzificha. Hedhi ni kitu cha kawaida unachotakiwa kujivunia nacho.

bottom of page