Mazingira Safi Maisha Bora
Karibu kwenye kampeni ya Mazingira Safi Maisha Bora, familia na jamii yako wamekuwa wakikusubiri! Kwa pamoja tunaweza kuwa na jamii ya kisasa na salama tunayoihitaji ambapo kunakuwa na utunzaji salama wa vyoo na taka ngumu, ili kuweka jamii zetu safi na mbali na magonjwa.
Hii ni nafasi yako kujifunza kuhusu tabia salama za usafi wa mazingira na faida zake. Jumuika nasi, unasubiri nini?
“Binafsi mradi huu umenifanya kuwa na shahuku ya usafi wa mazingira, na kuyafanya mazingira yawe safi na salama kwa ujumla. Umeniongezea uelewa kuhusu usafi wa mazingira”
Angel Mwaipopo - Afisa maendeleo ya jamii Manispaa ya Shinyanga
"Tunaishukuru SNV kwa kuboresha cha shule yetu, tulikuwa tunatumia choo kimoja wakati wanafunzi walikuwa wengi, kwa sasa ni afadhali, hivyo kwa niaba ya wanafunzi wenzangu ningependa kuwashukuru sana, na waendelee kufanya kile wanachokifanya kwenye mradi huu"
Kiranja mkuu shule ya Msingi Twendepamoja